Mkutano wa 40 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika umeichagua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwa kipindi cha miaka miwili (2022-2024) kwenye uchaguzi uliofanyika leo tarehe 3 Februari 2022. Tanzania imepata kura 43 kati ya kura 51 zilizopigwa.