Tarehe 29 Septemba Hadi tarehe 3 Oktoba, 2025 Johansburg, Afrika Kusini unafanyika mkutano wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wanaosimamia masuala ya Fedha Uchumi na Utengamano (8th Ordinary Session of the STC on Finance, Monetary Affairs, Economic Planning and Integration) wenye kauli mbiu " Bridging Africa's Health Financing Gap in a Changing Geo - Economic Context: Challenges and Potential Solutions" Kwenye mkutano huo, ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaongozwa na Mhe. Amina Kh. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muingano wa Tanzania ambaye amemwakilisha Waziri Fedha. Mhe. Naibu Katibu Mkuu ameambatana na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Afya na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ethiopia na Uwakilishi wa Kudumu kwenye Umoja wa Afrika. Lengo kuu la mkutano huo ni kujadiliana kuhusu mikakati ya pamoja ya kuziba pengo la ufadhili wa masuala ya Afya barani Afrika. Vilevile,  nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika watakubaliana kusuhu mabadiliko mapya ya kiuchumi duniani na hatuanza kuyakabili.