Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewasili Addis Ababa, Ethiopia leo tarehe 4 Februari 2022 kwa ajili ya kumwakilisha Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 5-6 Februari 2022.