Bi. Consolata Mushi, Mtendaji Mkuu wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) yupo kwenye ziara ya kikazi nchini Ethiopia kuanzia tarehe 01-07 Februari 2022. Katika ziara hiyo, Bi. Consolata Mushi amekutana na viongozi wa Jumuiya ya Wazungumzaji wa Kiswahili nchini Ethiopia (Ethiopian Swahili Community). Katika mazungumzo yao, wamekubaliana kushirikiana katika kuendeleza na kukuza matumizi ya Lugha ya Kiswahili nchini Ethiopia. Aidha, BAKITA ilipatia Jumuiya hiyo kitabu cha mwongozo wa kufundishia, kitabu cha kijifunza hatua ya awali na Kamusi ya Kiswahili.
BAKITA kushirikiana na Ethiopian Swahili Community kuendeleza na kukuza matumizi ya Kiswahili nchini Ethiopia
Bi. Consolata Mushi, Mtendaji Mkuu wa BAKITA (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ethiopian Swahili Community
