Leo tarehe 06 Mei 2022 Mheshimiwa Innocent Shiyo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ethiopia amewakaribisha  Ubalozini Wasanii wa Kimataifa kutoka Tanzania, Diamond Platnumz na Rayvanny. Balozi Shiyo amewapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya kupitia sanaa na mchango wao kwenye diplomasia ya utamaduni. Wasanii hao wanatarajia kutumbuiza tarehe 07 Mei 2022 Ghion Hotel-Addis Ababa nchini Ethiopia.