Tarehe 24 -28 Februari, 2025, Ubalozi wa Tanzania, Addis Ababa, uliungana na watumishi wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wanaohusika na masuala ya Siasa, Amani na Ulinzi (AUC – PAPs) na Baraza la Amani na Usalama la AU (PSC) katika Warsha iliyoandaliwa na Jumuiya ya nchi zinatumia lugha ya Kifaransa katika Umoja wa Afrika (the organisation Internationale de la Francophonie ‘(OIF). Warsha hiyo iliandaliwa mahsusi kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa wanadiplomasia wanaohusika katika kupanga, kusaidia, kusuluhisha, kutatua na kudhibiti migogoro Afrika.