Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 17 wa Kamati ya Kisekta ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Umoja wa Afrika  (African Union Specialized Technical Committee of Chiefs and Heads of Defense, Security and Safety-STCDSS) unaofanyika leo tarehe 11 Mei 2022 Jijini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo unajadili ushirikiano miongoni mwa nchi za Afrika katika masuala ya ulinzi na usalama ikiwemo mikakati ya kupambana na matishio ya usalama mathalan ugaidi na uhalifu unaovuka mipaka.