Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP. Simon Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Ethiopia, Kamishna Jenerali Demelash Gebremichael. Viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia katika masuala ya ulinzi na usalama. Mazungumzo hayo yamefanyika Jijini Addis Ababa, Ethiopia katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia.