Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa 14 wa Kamati Maalum ya Mawaziri wanaosimamia masuala ya Ulinzi na Usalama wa Umoja wa Afrika unaofanyika leo Jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 12 Mei, 2022.  Mhe. Waziri Dkt. Tax ameongozana na Mhe. Hamad Masauni Yusuf (Mb.) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania katika vikao vya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama uliofanyika tarehe 11 Mei 2022.