Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.), Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Nane wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika uliofanyika Accra, Ghana tarehe 28-29 Januari 2022. Mhe. Waziri Dkt. Ashatu Kijaji amelithibitishia Baraza hilo la Mawaziri nia ya Tanzania kuona Mkataba huo wa AfCFTA unakuwa chachu ya kuongeza fursa kwa nchi za Afrika kupanua zaidi biashara baina yao na kukuza uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya Bara la Afrika.

  • Mhe. Waziri Dkt. Ashatu Kijaji akifuatilia mjadala kwenye Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Umoja wa Afrika