Tarehe 14 Januari 2022 Mhe. Innocent Shiyo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Afrika UNECA alikutana na  kufanya mazungumzo na Mhe. Mohammed Arrouchi, Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Morocco kwenye Umoja wa Afrika na UNECA.  Mabalozi hao walikubaliana kushirikiana katika masuala yanayohusu Tanzania na Morocco (Bilateral Relations) na kwenye masuala ya Umoja wa Afrika na UNECA yenye maslahi kwa nchi zote mbili.