Ujumbe kutoka Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu watembelea na kufanya mazungumzo na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Addis Ababa tarehe 15 Septemba, 2021. Ujumbe wa Mahakama uliongozwa na Rais wa Mahakama ya Afrika, Mhe. Jaji Iman D. Aboud.
Mazungumzo yalijikita katika kuimarisha uhusiano kati Mahakama na Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika, nafasi ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu katika kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Umoja wa Afrika na namna ya kushughulikia changamoto zinazoikabili Mahakama hiyo.

