Lugha ya Kiswahili imechaguliwa kuwa lugha rasmi kutumika katika mikutano yote itakayoendeshwa na Umoja wa Afrika (AU). Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula amesema siku za nyuma kilikuwa kinatumika kama lugha ya kazi na katika ngazi ya mikutano ya marais tu.