Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia umeridhia Kiswahili kuwa Lugha ya Kazi ya Umoja wa Afrika. Ajenda ya kupendekeza Kiswahili kuwa Lugha ya Kazi iliwasilishwa na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuungwa mkono na nchi zote za Umoja wa Afrika.