On 26 November 2026, Tanzania’s Minister for Constitution and Legal Affairs, Hon. Abdallah Hamis Ulega (MP), chaired the 12th meeting of the African Union (AU) Specialized Technical Committee on Justice and Legal Affairs at AU headquarters in Ethiopia.

Ministers adopted legal instruments to create shared frameworks and guidelines, strengthen cooperation, and support effective implementation of legal matters across Africa.

The meeting included justice ministers and attorneys general from 34 African countries, demonstrating member states’ commitment to stronger legal systems, cooperation, and the rule of law.

MHE. ULEGA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA MAWAZIRI WA SHERIA YA UMOJA WA AFRIKA ADDIS ABABA

Leo tarehe 26 Novemba 2026, Mhe.Abdallah Hamis Ulega (Mb), Waziri wa Katiba na Sheria 🇹🇿 ameongoza Mkutano wa 12 wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali wa Umoja wa Afrika, uliofanyika Addis Ababa, 🇪🇹.

Mkutano huo umejadili na kupitisha nyaraka mbalimbali za kisheria zinazolenga kuweka mifumo na miongozo ya kisheria itakayotumiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika kuimarisha ushirikiano na utekelezaji wa masuala ya kisheria katika Bara la Afrika.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali kutoka nchi wanachama 34 ikiwa ni mwitikio katika kutekeleza kusudio husika.