Tarehe 26 March 2024, Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania (CSC) wakiongozwa na Col Jafari Ramadhani Aristide wakiwa katika ziara ya kimafunzo nchini Ethiopia walitembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia kwa ajili ya kusaini Kitabu na kupata Historia fupi ya Ubalozi sanjali na majukumu yake. Wakiwa Ubalozini walipokelewa Maafisa Ubalozi wakiongozwa na Mr. Frank Mwega, Mkuu wa Utawala Ubalozini (HoC) ambaye alimwakilisha Mhe. Balozi Innocent E. Shiyo ambaye yupo nje ya kituo cha kazi kushiriki majukumu mengine.